Ungana na Mchungaji mwenyeji, Askofu Mkuu Dr. Brown Mwakipesile katika ibada.
Siku ya jumatano jioni kuanzia saa 10:15 - 12:30 jioni, na kwa siku ya
Jumapili; English service kuanzia saa 01:30 - saa 02:45 asubuhi, ibada ya wote kuanzia saa 03:00 - 06:30 mchana na jioni kuanzia saa 10:15 - 12:30 jioni
Je unataabika na kuhangaishwa na dunia? Karibu EAGT Mlimwa West...
YESU KRISTO anatua mizigo yote, ukiwa hapa, utasaidiwa kurudi kwa Mungu, utapokea shuhuda mbalimbali kutoka kwa wengine zenye kutia na kuimarisha moyo, na mengine mengi
Fungua moyo wako, anza maisha mapya sasa
Mlimwa West ni famili ya Kikristo. Tunajali na kushughulikia mambo ya kiroho kwa watu wote.
Update Required
To play the media you will need to either update your browser to a recent version or update your Flash plugin.
UMISHENI
Umisheni wetu katika kanisa la EAGT Mlimwa West ni kuihubiri injili na kuwasaidia watu wote namna ya kumrudia Mungu na kuishi maisha matakatifu wapewayo kuyaishi kwa msaada wa Roho Mtakatifu
Tutembelee
Tunakaribisha wageni kutoka duniani kote kushiriki na sisi na kuishuhudia nguvu ya Mungu ikitembea katika ibada.
Mlimwa West ni kanisa shirikishi. Tunawapenda watu wote, tunajifunza na kukuza mahusiano mema. Hapa utakutana na idara shirikishi kama vile idara ya wamama, wababa, vijana n.k
Maombi ya wokovu
Ikiwa ungependa kuokoka umpokee YESU KRISTO katika maisha yako tujulishe, tutasimama imara kwa imani na wewe popote ulipo