(Huu ni msimamo wa kanisa letu kama kanisa la mahali pamoja)
USHIRIKA KATIKA KANISA LA EAGT MLIMWA WEST
ILI UKUBALIWE KUWA MSHIRIKA WA KANISA NA KUHUDUMIWA KIROHO ZINGATIA KUFANYA YAFUATAYO:-
Hakikisha kuwa umeokoka na kujitenga kabisa na dhambi na kuishi maisha matakatifu. Maisha ya utakatifu ndiyo mafundisho ya msingi ya kanisa hili [1 petro 1:15-16]
Hakikisha kuwa umebatizwa katika maji mengi.
Hakikisha kuwa umejazwa na Roho Mtakatifu na kunena kwa Lugha.
Hakikisha kuwa unalipa zaka kwa uaminifu kama Neno la Mungu lisemavyo (Mal. 3:10 )
Hakikisha unashiriki Ibada mara kwa mara.
Hakikisha unashiriki kutoa sadaka na michango kwa kadri Mungu anavyokujalia.
Hakikisha unachukua barua ya safari kwa safari unazosafiri kwa usalama wako.
Kama bado haujampokea Yesu Kristo kama Bwana na mwokozi wa maisha yako na unahitaji kufanya hivyo unaweza
kuwasiliana na Mchungaji kupitia namba ya simu +255 (0) 754 267 748 au +255 (0) 653 603 649.